Thursday, October 25, 2012

VIJANA KATIKA KUPAMBANA NA KIFUA KIKUU NA UKIMWI.

Ugonjwa wa kifua kikuu umekuwepo tangu enzi za mababu wakati UKIMWI umeanza miaka ya karibuni. Hata hivyo inajionyesha waziwazi na tafiti zimedhibitisha kuwa ugonjwa wa kifua kikuu umeongezeka mara dufu baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa UKIMWI.
Taarifa za shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa theluthi ya watu wote duniani wana maambukizi ya kifua kikuu na takribani watu milioni nane hupata maambukizi mapya kila mwaka, huku kukiripotiwa kuwa na vifo vya watu milioni mbili kila mwaka.
Taarifa hii anonyesha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya maambukizo haya yako katika nchi za Afrika na hasa kusini mwa jangwa la sahara. Tukumbuke kuwa Tanzania iko katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara.
Kifua kikuu kimezidishwa na virusi vya UKIMWI kwa sababu wadudu wa kifua kikuu hushambulia watu wenye upungufu wa kinga mwilini. Virusi vya UKIMWI hushambulia kinga ya mwili na hivyo kutoa nafasi kwa bacteria wa kifua kikuu kuibuka.

Wakati wadudu wa kifua kikuu huingia mwilini kwa njia ya hewa, Virusi vya UKIMWI huingia kwa njia ya kufanya mapenzi bila kinga, kuongezewa damu iliyo na virusi, kuchangia vitu vyenye incha kali na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Hata hivyo kuna sababu nyingi sana za kushuka kwa kinga ya mwili ikiwa ni pamoja na lishe duni, magojwa mengine kama malaria, saratani, homa ya matumbo na kadhalika. Napenda kuweka wazi kuwa si kila mwenye kifua kikuu atakuwa na virusi vya UKIMWI au UKIMWI wenyewe.
Kwa hiyo msomaji wangu kuwa huru kufikiria upya kwenda kupima  virusi vya UKIMWI kwani itakusaidia kupona haraka iwapo itagundulika kuwa una virusi vya UKIMWI. Napenda kukumbusha kuwa kifua kikuu ni kati ya magonjwa nyemelezi ya virusi vya UKIMWI kama ilivyo kwa magonjwa ya ngozi, fungus, malaria na kadhalika.
Vijana wa kundi la MUKIKUTE (Mpango wa mapambano dhidi ya Kifua kikuu na UKIMWI Temeke).Kundi hili lilianzishwa mwaka 2008,ambalo mpaka sasa lina washiriki 12.KUndi hili linajihusisha na muziki wa kiasili.Ni vijana ambao wanashirikiana na manispaa ya wilaya ya Temeke katika uhamasishaji na uelimishaji juu ya kifua kikuu na UKIMWI.Wamekuwa wakielimisha jamii kwa njia ya maigizo ya jukwaani pamoja na nyimbo au muziki wa kiasili wanaopiga.Ni mafanikio makubwa yanayoonekana katika wilaya hiyo kutokana na watu wengi kujitokeza katika vituo husika vya afya na kupima afya zao,na kupata elimu zaidi juu ya magonjwa haya hatari ya UKIMWI pamoja na kifua kikuu.Jamii nzima ya watanzania inashauriwa kuhudhuria katika vituo vya afya ili kupata uhakika wa afya zao,na kupata matibabu husika na ushauri nasaha endapo watagundulika kuambukizwa magonjwa haya hatarishi katika nyakati hizi barani Afrika na ulimwenguni kote.

Wednesday, October 24, 2012

Mojawapo ya njia zinazo tenganisha mitaa ya jijini Dar es Salaam.

Usafi Wa Mazingira

Usafi wa mazingira ni njia ya kuendeleza afya kwa njia ya kuzuia mawasiliano ya binadamu na athari za taka.Athari zinaweza kuwa za kimwili,mikrobiyolojia,biyolojia au kemikali vikolezo vya ugonjwa.

Taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na wanyama,taka ngumu,maji machafu,taka za viwandani na taka za kilimo.usafi kama njia ya kuzuia magonjwa unaweza kutumika kwa ufumbuzi handisi (kama maji taka na matibabu ya maji machafu),teknolojia rahisi kama vyoo,au matendo ya usafi binafsi kama uoshaji wa mikono kwa sabuni.Usafi wa mazingira kama inavyoelezwa kwa ujumla na Shirika la Afya Duniani (World Health Organisation),inahusu utoaji wa vifaa na huduma ya usalama wa mkojo na kinyesi cha binadamu.Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote.Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kuzuia athari athari za uchafu katika kaya na katika jamii.Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi wa mazingira


,kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa taka na maji machafu.Utupaji wa taka ngumu hufanyika katika mashimo ni kawaida iliyofanywa.Umuhimu wa kufukia taka ni kwa upungufu wa kueneza magonjwa na visababishi vya ugonjwa.Ufukiaji wa kila siku pia hupunguza uenezo wa harufu ya taka kwasababu ya upepo,katika nchi zilizoendelea ni sharti kufukia kufanywe kwa njia mwafaka,kwa mfano peerimeta ya mchanga inafaa kutumiwa ili kupunguza uchafuzi wa maji ya kunywa.Lililo la msingi zaidi na lakuzingatiwa ni kutotupa taka ngumu au taka za aina yoyote karibu na makazi ya watu kuepusha mgonjwa ya mlipuko kwa jamii.


Monday, October 22, 2012

BIASHARA NDOGONDOGO.



Tanzania ni nchi mojawapo katika nchi tatu zinazoongoza kwa kasi ya kukua,kutokana na takwimu za vyama vya kimataifa.Na pia kutokana na takwimu hizo pia zinaonyesha uchumi wa bara la afrika unakua kwa kasi zaidi kuliko mabara mengine.

thumekua tukishuhudia watanzania wengi sasa wakijihusisha na ujasiriamali kwa kuanzisha biashara ndogondogo zinazowapatia kipato.
Bwana Abubakari Fikiri (31) maarufu kwa jina la 'Fundi Abuu',amekua akijishughulisha na shughuli za ushonaji nguo kwa mwaka wa tatu sasa.Alisema kuwa,kazi hiyo inamsaidia kupata kipato anachoweza kujikimu mahitaji yake yote na familia yake,kama alivyoeleza akiwa mtoni kijichi,jijini Dar es Salaam.

Katika banda hili,huuzwa vitu vya kiasili kama vile vikapu,vikoi,michoro mbalimbali na urembo kama vile hereni na vingine vingi.Bidhaa hizi huandaliwa na wabunifu na wajasiriamali wa kikundi cha Umoja wa jijini Dar es Salaam

Bwana Selemani Idd (28),ni mjasiriamali anaeuza viazi ulaya katika soko la mtongani wilaya ya temeke, jijini Dar es Salaam.

Inafurahisha na kuleta matumaini sana kuwaona ndugu zetu hawa wa jijini Dar es Salaam walivyoamua kutumia ubunifu,ujuzi na bidii bila kukata tamaa.Hawakujali hali waliyo kua nayo na kuanzisha biashara ndogondogo kwa malengo ya kufanikiwa.Hii ni changamoto kwa watu wote,ili taifa liendelee na kukua kiuchumi ni lazima tuwe wabunifu na kujituma bila kukata tamaa katika hali yoyote.
.

Monday, October 8, 2012

Kijana Abdul Mohamed wa kundi la T.Afrika akionyesha umahiri wake katika sarakasi.
Vijana wa kikundi cha T.Afrika wanaojishughulisha na kucheza ngoma za asili na sarakasi,pia ni washindi wa shindano la Dance Mia Mia (2012)  lililoanzishwa na televisheni ya East Africa
Dar es Salaam ni jiji  maarufu linalotambulika kibiashara,lakini wakazi wa pembezoni mwa jiji hili wamekua wakijihusisha na kilimo cha bustani ndogo ndogo kwa mahitaji ya kila siku.